Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Monday
Sep 06th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Local General Ushahidi kesi ya Jerry Muro wakamilika

Ushahidi kesi ya Jerry Muro wakamilika

Mwandishi wa habari wa TBC, JERRY MURO

Upelelezi wa kesi inayomkabili mwandishi wa habari wa TBC, JERRY MURO, na wenzake wawili, EDMUND KAPAMA, na DEOGRATIUS MGASSA ambao ni wafanyabishara umekamilika na kesi hiyo itaanza kusikilizwa tarehe Kumi na Nne mwezi ujao wa Juni mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi KISUTU.

Hatua hiyo imekuja Baada ya upande wa mashtaka ukiongozwa na MARTHA MISONGE, kueleza kwamba upelelezi wa shauri hilo umekamilika, na  ndipo Hakimu mkazi GABRIEL MIRUMBE, alipoeleza kwamba watuhumiwa watasomewa maelezo yao ya awali.

Inadaiwa kuwa tarehe Ishirini na Tisa mwezi Januari mwaka huu jijini DSM, watuhumiwa hao walikula njama, kuomba rushwa ya Shilingi Milioni KUMI kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya BAGAMOYO MICHAEL WAGE, na ambapo washtakiwa MGASA na KAPAMA walijifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa –TAKUKURU.

Inadaiwa kuwa washtakiwa waliomba rushwa hiyo baada ya kumtishia WAGE kwamba habari zake za ubadhirifu wa fedha za umma kama Mhasibu wa halmashauri zitatangazwa kwenye luninga.

Last Updated ( Wednesday, 02 June 2010 08:15 )  
Banner