Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Thursday
Sep 09th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Local General Miradi iendane na thamani ya fedha-Kombani

Miradi iendane na thamani ya fedha-Kombani

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI CELINA KOMBANI

Wakati Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti wa hesabu za Serikali nchini ikijiandaa kuanza kutumia utaratibu mpya wa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika ngazi za wilaya na mikoa kwa lengo la kulinganisha ujenzi huo na kiwango cha fedha kilichotumika, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI CELINA KOMBANI amezungumzia tatizo hilo na kulioanisha na mtindo wa kulindani ambao amesema umeanza kujengeka katika baadhi ya ngazi za uongozi nchini

Waziri KOMBANI amesema hayo mbele ya wandishi wa habari Jijini DSM alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na ofisi zilizo chini ya TAMISEMI ambapo ameeleza kuwa fedha nyingi zinazopelekwa kwenye miradi ya maendelea hazilingani na thamani ya baadhi ya miradi inayojengwa.

Last Updated ( Thursday, 03 June 2010 06:41 )  
Banner