
Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, SEIF SHARRIF HAMAD, ametangaza nia yake ya kugombea nafasi ya urais wa
Hii ni mara ya NNE kwa Kiongozi huyo, pamoja na mwenyekiti wa CUF Taifa, IBRAHIM LIPUMBA, ambaye naye ametangaza nia ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA juzi, kuwania nafasi hizo.
Hekaheka za maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao zimeanza kushuika kasi kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ambapo hii leo Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim SEIF SHARIFF HAMAD ameweka bayana nia yake ya kuwania Urais wa serikali ya Mapinduzi ZANZIBAR ikiwa ni miezi mitano kabla ya kinyang’anyiro hicho kufanyika.
Akitangaza azima yake hiyo mbele ya Waandishi wa Habari mjini DSM Maalim SEIF amesema dhamira yake hiyo ni thabiti.
Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CUF taifa Profesa IBRAHIM LIPUMBA ambaye ametoa rai kwa tume ya uchaguzi kisiwani ZANZIBAR –ZEC- kuhakikisha kuwa wananchi wanapatiwa fursa ya kujiandikisha bila kuwekewa mizengwe.
Aidha Mwenyekiti huyo wa CUF ametoa rai kwa wabunge kuhakikisha kuwa wanashiriki vema katika mchakato wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2010 – 2011 na kuhakikisha kuwa bajeti hiyo inakuwa bora na kuwa chachu ya maendeleo na ustawi wa wananchi .



