Waathirika wa mafuriko Rufiji wapewa chakula, boti

0
136

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amefika Wilayani Rufiji, mkoani Pwani kuwafariji waathirika wa mafuriko na amekabidhi tani nne za chakula na boti pamoja na mashine yake ili viwasaidie waathirika hao.

Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga Mkoa huo wa Pwani amekabidhi vitu hivyo leo Aprili 11, 2024 kwa Mbunge wa Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa aliyepokea kwa niaba ya wananchi wa Rufiji waliopatwa na mafuriko.