Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Monday
Sep 06th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Kenya Palestina yatangaza siku 3 za maombelezo

Palestina yatangaza siku 3 za maombelezo

Kiongozi wa mamlaka ya PALESTINA MAHMOUD ABBAS

Kiongozi wa mamlaka ya PALESTINA MAHMOUD ABBAS, ametangaza siku tatu za maombolezo, baada ya watu 16 waliokuwa kwenye meli zinazopeleka misaada PALESTINA, kufa baada ya  mapambano baina ya abiria na makomandoo wa ISREL, waliovamia msafara wa meli hizo.

 Tukio hilo limesababisha hasira kutoka UTURUKI, na wanamgambo wa kikundi cha HAMAS cha PALESTINA,  ambacho kimetaka mamlaka ya PALESTINA, kusimamisha mazungumzo kati yake na ISRAEL.

 UTURUKI imesema uvamizi wa ISRAEL, dhidi ya msafara wa meli ambazo baadhi zinatoka nchini UTURUKI, unaweza kuharibu vibaya uhusiano baina ya nchi hiyo mbili.

 Jeshi la ISRAEL limethibitisha vifo vya wanaharakati wanaounga mkono WAPALESTINA, ambapo askari wake wanne pia wamejeruhiwa. Taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari imesema makamondoo wa ISRAEL, walifyatua risasi baada ya kushambuliwa kwa visu na mashoka, na abiria waliokuwa kwenye meli iliyokuwa imebeba misaada kuelekea PALESTINA.

 
Banner