Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Thursday
Sep 09th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Kenya Santos aongoza uchaguzi Columbia

Santos aongoza uchaguzi Columbia

Waziri wa Ulinzi wa zamani wa columbia JUAN MANUEL SANTOS

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais uliofanyika hapo jana nchini COLOMBIA yanaonyesha kuwa Waziri wa Ulinzi wa zamani wan chi hiyo  JUAN MANUEL SANTOS  anaongoza kwa kupata asilimia Arobanini na Sita ya kura zote zilizokwishahesabiwa.

Kulingana na matokeo hayo MANUEL ambaye ni mrithi wa Rais ALVARO URIBE anayeondoka madarakani baada ya muda wake kumalizika atakabiliwa na duru ya pili ya uchaguzi itakayofanyika tarehe Ishirini ya mwezi ujao.

Kwa mujibu wa matokeo hayo ya awali yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya COLOMBIA, mpinzani mkubwa wa MANUEL - ANTANAS MOCKUS ambaye ni meya wa zamani wa BOGOTA amepata asilimia Ishirini na Moja ya Kura zilizokwishahesabiwa.

Matokeo hayo yanaonyesha huenda wagombea hao wakashindwa kupata kura zitakazowawezesha kuwa washindi wa moja kwa moja hivyo kuhitaji duru ya pili ya upigaji kura ili aweze kupatikana mshindi.

 
Banner