Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Thursday
Sep 09th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Kenya Poland kutangaza siku ya uchaguzi leo

Poland kutangaza siku ya uchaguzi leo

Kaimu Rais wa POLAND,BRONISLAW KOMOROWSKI

Kaimu Rais wa POLAND ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la nchi hiyo BRONISLAW KOMOROWSKI leo Jumatano anatarajiwa kutangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais kufuatia kifo cha rais KACZYNSKI.

Kwa mujibu wa katiba ya POLAND, KOMOROWSKI ana siku kumi na nne za kutangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais tangu kufariki kwa rais ambapo uchaguzi huo utafanyika ndani ya siku sitini tangu kutangazwa kwa tarehe ya uchaguzi.

Uongozi huo wa serikali ya POLAND umesema misa ya mazishi ya Rais LECH KACZYNSKI na mkewe itafanyika Jumamosi ijayo

Uongozi huo umeseme tayari familia ya marehemu imechagua eneo ambalo miili ya marehemu hao itazikwa na kusema ni mapema kueleza sehemu ambapo kiongozi huyo na mkewe watazikwa.

Rais LECH KACZYNSKI amekufa Jumamosi iliyopita wakati ndege iliyokuwa imemchukua pamoja na ujumbe wa serikali yake kupata ajali Magharibi mwa URUSI wakati ujumbe huo ukienda kuadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya askari wa POLAND waliouawa nchini URUSI wakati wa vita vya pili vya dunia.

Last Updated ( Thursday, 15 April 2010 07:17 )  
Banner