
Wakati askari wakijaribu kuchukua maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na waandamanaji wanaopinga serikali ya THAILAND, zaidi ya watu 15 wamekufa na wengine mia tano kujeruhiwa katika mapigano yaliyofanyika katika mji mkuu wa THAILAND, BANGKOK.
Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao ambao nao walitupa mabomu ya petroli.
Waziri Mkuu wa THAILAND, ABHISIT VEJJAJIVA amesema jeshi nchini humo limesitisha operesheni zake.
Waandamanaji ambao wameweka kambi katika maeneo mbalimbali ya mji wa BANGKOK kwa takriban mwezi mmoja sasa wanataka uchaguzi ufanyike mapema.