Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Monday
Sep 06th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Kenya PUTIN atembelea eneo lililotokea ajali

PUTIN atembelea eneo lililotokea ajali

Waziri Mkuu wa URUSI, VLADIMIR PUTIN

Waziri Mkuu wa URUSI, VLADIMIR PUTIN ametembelea eneo ambalo ndege iliyokuwa na watu zaidi ya 100 kutoka POLAND ilianguka na kuwaua wote akiwemo Rais LECH KACZYNSKI wa POLAND na kusema atahakikisha uchunguzi wa kina unafanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Habari za awali zinasema marubani hawakuzingatia ushauri uliotolewa na waongoza ndege wa kuwataka kwenda kutumia uwanja mwingine wa ndege kutokana na hali mbaya ya hewa huko SMOLENSK nchini URUSI.

Miongoni mwa abiria walikuwemo kwenye ndege hiyo ni Mkuu wa majeshi na gavana mkuu nchini POLAND.

Siku saba za maombolezo zimetangazwa nchini humo.

Last Updated ( Monday, 12 April 2010 09:50 )  
Banner