Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Thursday
Sep 09th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home Kenya Rais Kurmanbek akimbia mji mkuu wake

Rais Kurmanbek akimbia mji mkuu wake

Rais wa KYRGYZSTAN,KURMANBEK BAKIYEV

Rais wa KYRGYZSTAN KURMANBEK BAKIYEV, aliyelazimika kuukimbia mji mkuu wa nchi hiyo BISHKEK, kufuatia ghasia za wananchi kupinga rushwa na gharama za umeme, amesisitiza kuwa hatajiuzuru wadhifa wake.

BAKIYEV amesema yeye ni Rais halali, ambapo amelaani ghasia zilizozuka  juzi na kudai kuwa watu wenye silaha, wamekuwa wakitembea katika mitaa ya mji mkuu wa KYRGYZSTAN, wakipora vitu.

Hata hivyo Rais huyo anayedai kuwa yuko Kusini mwa nchi hiyo, amesema yuko tayari kuzungumza na serikali ya mpito.

Upande wa upinzani ukiongozwa na Waziri wa mambo ya nje wa zamani nchini humo, ROZA OTUNBAYEVA, umetangaza kuchukua madaraka ya nchi hiyo.

Wakati huo  huo leo ni siku maalum ya maombolezo ya kitaifa, ya watu 75 waliopoteza maisha yao kutokana na ghasia, zilizozuka jumatano nchini KYRGYZSTAN.

Last Updated ( Monday, 12 April 2010 09:20 )  
Banner