
Rais Barack Obama wa Marekani, amekutana na askari wa nchi hiyo walioko nchini Afghanistan, na kuwaeleza kuwa wanawajibika kuhakikisha amani inapatikana nchini Afghanistan.
Akizungumza na askari na raia katika kambi ya Bagram, iliyoko karibu na mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, Obama amewashukuru kwa kazi wanayoifanya nchini humo, na kuongeza kuwa anataka kuona jitihada zinaendelea za kumaliza rushwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, huku Afghanistan ikiwa ni miongoni mwa nchi duniani zinazolima Opium, inayotengeneza dawa za kulevya aina ya Heroin.
Rais huyo wa Marekani amesema majeshi hayo, yako kwa ajili ya kuhakikisha Marekani inakuwa katika hali ya amani na usalama.
Obama ambaye hii ni mara yake ya kwanza kwenda nchini Afghanistan,amekwishaondoka nchini humo.