Watanzania na wapenda muziki wa dansi nchini
Maneti Ulaya alijiunga na bendi ya Vijana, mnamo mwaka 1975 na kupewa uongozi mwaka huo huo kutoka kwa John Ondolo Chacha aliyekuwa mmojawa wa viongozi waanzilishi. Maneti alitokea bendi ya TK Lumpopo ya Morogoro alipokuwa akiimba pamoja na Juma Kilaza (sasa marehemu).
John Ondolo Chacha alikuwa kiongozi wa kwanza wa bendi hii ambayo ilianzishwa kwa ushirikiano na Joseph Nyerere, ambaye alikuwa kaka wa muasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Maneti aliingia Vijana Jazz kwa kishindo kwani kwa muda mfupi tu aliweza kutoa vibao moto moto kadhaa ikiwa ni pamoja na “Niliruka Ukuta” , “Sabina” na “
Wakati Maneti anachukua uongozi Vijana Jazz ilikuwa inatumia mtindo wa Kokakoka. Nyimbo nyingine alizotunga Hemedi Maneti Ulaya akiwa na Vijana Jazz ni pamoja na Hekaheka Hekaheka, Huyo Anapata, Zuhura Naondoka, Kamata Ooh Sukuma, Mary Maria, Penzi Halina Umaarufu, Nimeruka Ukuta Namba Mbili, Operesheni Maduka, Matata Matata Oooh Matata Matata, Kwani Jiko Limenuna, Mundinde Acha Tabia Mbaya, Vijana Ndiyo Nguzo Na Jeuri Ya Chama, Bujumbura Iyo Burundi.
Nyingine ni Tambiko La Pamba Moto, Magaidi Wa Msumbiji, Mfitini Huyu Ni Nani, Mama Chichi, Rushwa Adui Wa Haki, Alli Hassan Mwinyi Apewe Kura Ya Ndiyo, Shoga Yangu, Chiku Mwana Mama, Mwisho wa Mwezi, Heshima ya Mtu Ni Kuolewa na Safari Yetu Zambia ambao bahati mbaya haukuweza kurekodiwa kutokana na hali ya maumivu makali aliyokuwa nayo Maneti kabla ya kufariki.
Wimbo wake mwingine wa ‘Mzee Tupatupa’ ingawa aliutunga zaidi ya miaka 30 iliyopita unaweza kulinganishwa na 'Mzee Fataki' leo hii kwa tabia zake za kujihusisha na mapenzi kwa wanafunzi.
Maneti alikuwa na kipaji cha kipekee cha uongozi alichojaliwa na Mwenyezi Mungu, kwani aliweza kuiongoza bendi ya Vijana Jazz tangu kujiunga hadi kifo chake mwaka 1990 bila kuyumba. Alitunga nyimbo za Siasa, Mapenzi, Utamaduni na zote ziliigusa jamii vilivyo.
Kutokana na uongozi wake mahiri Vijana Jazz iliweza kubadili mitindo yake ya dansi kutoka Koka Koka kwenda Takatuka, Heka Heka, Pamba Moto Awamu Ya Kwanza, Pamba Moto Awamu ya Pili, Pamba Moto Awamu ya Pili, Shambulia Bara hadi Pwani.
Baadhi ya nyimbo ambazo ingawa hakuzitunga Maneti alishiriki kuimba akiwa na bendi hiyo ya Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi ni pamoja na Tuwaheshimu Mama wa Kambo, Wifi Zangu Mna Mambo, Ogopa Tapeli uliotungwa na marehemu Adamu Bakari, Wivu ni Ugonjwa Jamani, Penzi Haligawanyiki Sehemu ya Kwanza uliotungwa na Kida Waziri, Macho Shingo Feni, Aza Umesaliti Penzi Langu, Penzi Haligawanyiki Sehemu Ya Pili na tungo nyinginezo zilizoiwezesha Vijana Jazz kuwa miongoni mwa bendi kubwa nchini zilizoweza kuchuana ubavu na bendi kama JUWATA Jazz “Msondo Ngoma”, Mlimani Park Orchestra, Magereza Jazz, Marquiz Du Zaire, Bima Lee na Polisi Jazz.
Maneti kutokana na kipaji cha uimbaji na uongozi aliweza kufanya kazi pamoja na wanamuziki wengi ambao baadhi yao bado wako hai kama Komandoo Hamza Kalala, Shaaban Yohana "Wanted", Kida Waziri “Stone Lady”, Max Bushoke, Rashid Pembe, Chris Sheggy, Mgonazeru, Saburi, Aggrey Ndumbalo, Cosmas Chidumule.
Kipaji cha Maneti kinaonekana wazi katika utunzi wake huu wa Mary Maria ambako anaonesha alivyomhusudu dada huyo Mary. Baadhi ya maneno ya Wimbo huo ni: Kwa kweli sasa nimenaswa
Sina ujanja eeeh eeeh,
Sina ujanja eehhh
Kupenda sawa na ajali
Haina kinga eeh eeh
Haina kinga eeh Nilivyomuhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliweeeee
Na wala sitapenda mpaka nife,
Mpaka nife, mama Mary oooh
Hili ni kasha la kaseti mojawapo iliyowahi kurekodiwa na bendi ya Vijana Jazz. Manet.
(Bendi ya Vijana Jazz aliyokuwa akiimbia Maneti).
Wanamuziki ambao walifanya kazi na Maneti ambao sasa ni marehemu ni pamoja na Athumani Momba, Adamu Bakari "Sauti ya Zege”, Jerry Nashon "Dudumizi", Suleiman Mbwembwe, Eddy Sheggy, Rahma Shally na Mohammed Gotagota.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Beno Malisa alipozungumza katika hafla ya siku ya kumbukumbu ya kiongozi huyo iliyofanyika Mei 31 mwaka jana katika ukumbi wa Vijana, Kinondoni, jijini Dar es Salaam alitoa changamoto kwa bendi ya Vijana Jazz kuendelea kumuenzi aliyekuwa kiongozi wa bendi hiyo, Hemed Maneti kwa kuendeleza tungo zenye maadili na busara kwa mashabiki wake.
Kwenye mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika
Ndipo Rais Jakaya Kikwete alipoahidi kuwa atairudishia hadhi bendi hiyo kwa kuwanunulia vyombo . Ikumbukwe kuwa mwaka 1985 wakati wa kumtambulisha Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, bendi ya Vijana ilizunguka nchi nzima kumtambulisha mgombea huyo na wimbo wao wa ‘Ali Hassan Mwinyi apewe kura ya ndiyo’.



