Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)

Monday
Sep 06th
Text size
  • Increase font size
  • Default font size
  • Decrease font size
Home About Tanzania Posta yaingia mkataba na Afikasana

Posta yaingia mkataba na Afikasana

Shirika la Posta Tanzania

Shirika la Posta Nchini TPC limeingia mkataba wa kibiashara na kampuni ya kutengeneza bidhaa za kiutamaduni ya AFRIKA SANA itakayowezesha kuuzwa kwa bidhaa hizo kwa watalii wanaotembelea mikoa mbalimbali

 

Ushirikiano huo utawapatia AFRIKA SANA nafasi ya kutangaza bidhaa zao za utamaduni wa kiafrika kwa wageni wanapotembelea ofisi za  posta na kurahisisha kuzituma nje ya nchi kwa njia ya posta na kwa upande mwingine SHIRIKA LA POSTA litafaidika kwa kuuza bidhaa zao za stampu katika vituo vya AFRIKA SANA

 

Akifungua semina elekezi kwa watendaji wa SHIRIKA la POSTA na AFRIKA SANAA, KAIMU POSTAMASTA MKUU KHAMIS MNDEME amesema wanatarajia kuziunganisha bidhaa za kiutalii za stempu zinazokusanya kumbukumbu za kihistoria na kijiographia kuwekwa karibu na vinyago, nguo na mapambo ya kiutamaduni wa kiafrika zinazotengenezwa na AFRIKA SANA.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi wa AFRIKA SANA NDESUMBUKA MERINYO amesema kujiunga na mtandao wa posta kutawarahisishia kazi ya kufungua maduka nchi nzima kuzitangaza bidhaa zao.

Last Updated ( Thursday, 02 September 2010 12:49 )  
Banner